Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya
Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah
Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada
ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke mara baada
ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke kufuatia
mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali ya Tanzania
kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera
kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi
Bilioni sita za Kitanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke kufatia mchango wa Waziri Mkuu wa Uingereza alioutoa kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kiasi cha Paundi za Uingereza Milioni 2.3 sawa na Takribani Shilingi Bilioni sita za Kitanzania. NA IKULU
RAIS John Magufuli amepokea zaidi ya Sh bilioni sita kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ndege mbili za Serikali, Rais Magufuli alisema alikabidhiwa fedha hizo jana asubuhi na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke.
Aidha, Rais Magufuli alisema wadau mbalimbali wametoa fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko hilo, lakini Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Amantius Msole pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda, waliamua kufungua akaunti inayofanana na iliyofunguliwa rasmi kwa ajili ya kukusanya fedha za msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko na kuanza kuzitafuna.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Katibu Tawala huyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba walikamatwa jana na kufikishwa mahakamani mjini Bukoba.
Kutokana na maelezo ya Rais, baada ya Serikali kuchukua hatua hiyo iliyowapa imani wadau mbalimbali wanaojitolea kuchangia walioathirika na tetemeko hilo, Ubalozi wa Uingereza ulichanga pauni milioni 2.3 zilizotolewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Rais Magufuli alieleza kuwa Uingereza na wadau wengine wamekuwa na imani zaidi kuwa fedha wanazotoa zinawafikia walengwa.
Juzi, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Kagera pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Manispaa hiyo ya Bukoba, baada ya viongozi hao kubainika kuwa walifungua akaunti nyingine inayofanana na ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya Maafa ya Kagera kwa ajili ya kujipatia fedha.
Viongozi hao wanadaiwa kufungua akaunti yenye jina “Kamati Maafa Kagera” linalofanana na la akaunti rasmi kwa lengo la kujipatia fedha kwa maslahi yao.
Aidha Rais amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei awachukulie hatua watumishi wa benki hiyo walioshirikiana na watumishi hao kufanya njama za kuanzisha akaunti nyingine ya benki yenye jina linalofanana na akaunti rasmi ya “Kamati ya Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha.”
0 comments:
Post a Comment