Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar.
Mh Salum Ussi Pondeza AMJADI leo alikuwa mgeni rasmin kwenye semina elekezi ya viongozi wapya wa UVCCM ngazi ya matawi wadi na jimbo wa Jimbo lake la Chumbuni semeni hiyo ilifanyika katika ukumbi wa CCM Jimbo la Chumbuni.
Mara baada ya kukaribishwa kufunguwa semina hiyo Mh Amjadi alisema.
Binafsi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia siku ya leo kuwa wazima na kuoata fursa ya kukutana kwa lengo la kupigana msasa kidogo tukumbushane wajibu na majukumu yetu ya msingi ya kikatiba na kikanuni ili ifike mahali tuache kufanya kazi kwa mazoea
Ndio vijana na amini nyote mnajuwa kuwa dunia imebadili tunalazimika na sisi tubadilike tuendane na wakati kabla mabadiliko hayajatulazimisha kubadilika.
Kwa kuktadha huo imeandaliwa semina ili vijana tujuwe wajibu wetu hasa kwa Chama unaposikia vijqna ndio jeuri ya Chama huwa hasemwi tu ovyo ni jeuri ya Chama kweli kweli hivyo leo hapa wakufuzi wapo watawapa muelekeo na mjitambuwe kuwa nyinyi ndio jeshi kamili la kuhakikisha CCM inarudi madarakani 2020 kwa vyovyote vile kama inavyo elekezaji katiba ya CCM ibara ya tano kifungu cha kwaza inapofika wakati wa uchaguzi hakuna mzaha.
Pia nichukuwe fursa hii kwa kuwapongeza nyote viongozi wapya mlio chaguliwa kwa ngazi zote mmetumia haki ya msingi ya kuchaguwa na kuchaguliwa niwaombe muwasongeze karibu mfanye kazi kwa pamoja na wale wote ambao walijaza fomu na kura hazikutosha maana hichi Chama si cha viongozi tu bali ni cha wanaccm wote awe mwanachama au kiongozi na mkifanya kazi kwa njia ya kushirikisha mtafanakio na UVCCM iliyo kimbilio kwa vijana wote Chumbuni na Tanzania nzima kwa ujumla itapatikana.
Mwisho niwambie sisi viongozi tupo kwa ajili yenu mimi na Mh Muwakilishi wetu tunawapenda tupo tayari kwa lolote tena bila ya cm na barua kukutokea jambo ambalo tunahitajika kulifanya tuqmbieni muda wowote Mh Muwakilishi wetu anawasalimia yeye yupo nje ya nchi kikazi na kwa ajili yenu pia
Mimi binafsi nilikuwa Dodoma kwa shuhuli za kibunge ila jana nililazimika kuja japo mara moja kuhakikisha semina yetu haikwami na baada ya kuifunguwa rasmin nitarudi Dar kidogo kumalizia majukumu imani yangu mtakuwa wasikivu ili wakufuzi muwaelewe vizuri sana.
Baada ya nasaha zangu izo chache natamka semeni elekezi hii nimeifunguwa rasmin
0 comments:
Post a Comment