Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es
Salaam limeendelea na msako wa wahalifu sehemu mbalimbal za Jiji hilo na
lufanikiwa kupatikana kwa silaha moja aina ya bastola na kuuwawa kwa
majambazi watatu.
Akizungumza na waandishi wa habari
Kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa
amesema Jeshi la Polisi kanda maalum mnamo tarehe 13 mezi wa 9 mwaka huu
majira ya saa tatu usiku huko Mbiku Chamazi lilifanikiwa kukamata
silaha moja, bastola aina ya BERRETA yenye namba A065775Z ikiwa na
risasi tano ndani ya magazine katika majibizano ya risasi kati ya Askari
Polisi na majambazi wapatao watano.
“Silaha hiyo ilipatikana baada ya askari kupata taarifa ya kuwepo kwa njama za majambazi hao watano (5) kufanya uporaji katika maduka ya M-Pesa na Tigopesa eneo hilo, na hatimaye kuweka mtego eneo hilo ambapo askari walifanikiwa kuwaona majambazi hao wakishuka kwenye gari yao kwaajili ya kufanya tukio hilo” Alisema Kamanda Mambosasa.
Vile vile Kamanda Mambosasa ameongeza kwa kusema kuwa kuwa majambazi hao walipogundua wanafatiliwa na askari walianza kufyatua risasi kuwashambulia askari na ndipo askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu kati ya watano huku wengine wawili wakikimbia.
Aidha Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa silaha hiyo aina ya bastola baada ya kupekuliwa, risasi tano zilikuwa ndani ya magazine, moja ilikuwa chemb tayari kwa kutoka huku maganda sita ya silaha hiyo yalipatikana eneo la tukio, huku majambazi waliojeruhiwa walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali ya Taifa Muhimbili ili kupatiwa matibabu, huku msaka mkali ukiendelea kuwatafuta majambazi wawili walio kimbia.
Kamanda Mambosasa pia ametoa katazo la mikusanyiko isiyo na kibali kutoka Polisi na ametoa onyo kali kwa watakaokiuka kwani hatua kalii za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
0 comments:
Post a Comment