RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dk
Magufuli amesema katika mazungumzo yao, wamezungumza mambo mbalimbali
ikiwamo kumtakia heri Dk Shein ambaye jana aliadhimisha siku yake ya
kuzaliwa.
Naye Dk Shein alisema anamshukuru Dk Magufuli kwa kumtakia heri
katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana
mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.
“Mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana, lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana,” alieleza Dk Shein.
Alisema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Magufuli ili
wabadilishane mawazo, kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Tuesday, March 14, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Anna Joram Gidarya, amewataka wananchi wa Wilaya ya Busega kutoa maoni kwa uhuru kuhusu ombi la k...
-
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi mkoani Iringa wakati wa z...
-
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Laigwnani Metui Ole Shaudo mapendekezo ya Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro kuhusu namna bor...
-
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa Na Mathias C...
Powered by Blogger.

0 comments:
Post a Comment