RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dk
Magufuli amesema katika mazungumzo yao, wamezungumza mambo mbalimbali
ikiwamo kumtakia heri Dk Shein ambaye jana aliadhimisha siku yake ya
kuzaliwa.
Naye Dk Shein alisema anamshukuru Dk Magufuli kwa kumtakia heri
katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana
mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.
“Mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana, lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana,” alieleza Dk Shein.
Alisema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Magufuli ili
wabadilishane mawazo, kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.

No comments:
Post a Comment