METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, March 14, 2017

Magufuli, Shein wateta Chamwino

RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dk Magufuli amesema katika mazungumzo yao, wamezungumza mambo mbalimbali ikiwamo kumtakia heri Dk Shein ambaye jana aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Naye Dk Shein alisema anamshukuru Dk Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.

“Mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana, lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana,” alieleza Dk Shein.

Alisema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Magufuli ili wabadilishane mawazo, kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com