Wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji wanatakiwa kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo aliyasema hayo jana Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje
kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji
pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi
mabadiliko ya hali halisi ya vileo.
“Pombe
za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria
ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara
wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa
kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa
5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi
hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.
Vile
vile alisema kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni tabia ya mtu ambayo
inawezekana kabisa haitokani na mapungufu ya Sheria.
Hata
hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameagizwa kusimamia taratibu za
uendeshaji wa biashara za vileo na kuchukua hatua kwa watumiaji na
wafanyabiashara wanaobainika kukiuka Sheria hiyo.
Aidha
alisema kuwa, endapo ipo haja ya kuifanyia marekebisho Sheria ya vileo,
Serikali itakuwa tayari kupokea mapendekezo kwa eneo ambalo litaonekana
kuwa na mapungufu ili kufanyiwa marekebisho kupitia Bunge.
Jafo
alitoa wito kwa Watanzania wote kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii
ili kujiletea maendeleo kwa ustawi wa Taifa zima. Aidha Serikali
haitasita kuchukua hatua kwa wanywaji pombe wasiozingatia utaratibu
pamoja na wazururaji wakati wa kazi.
0 comments:
Post a Comment