Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani
Jafo akizungumza katika hafla ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Leo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu
Chaula akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Joseph Semboja akiwasilisha taarifa
ya awali kwa Mgeni Rasmi na Washirki wakati wa kufungua mafunzo ya
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma
Leo.
Baadhi
wa wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
walioshiriki kwenye mafunzo ya uongozi yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais
Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
Katika
picha ya pamoja ni Naibu Waziri wa OR-Tamisemi Selemani Jafo (mbele
katikati), Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt. Zainabu Chaula (mbele
kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja
(mbele kulia) pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi
walioandaa mafuno haya.
……………………..
Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi ili kutimiza matarajio ya watanzania ambao
wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi
wa Serikali ya awamu ya Tano.
Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za
Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa
na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano na
Taasisi ya Uongozi.
Akiungumza katika ufunguzi wa
mafunzo hayo Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia Wananchi kwa
kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku
wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya
kazi na kuhakikisha hakuna muingiliano wa majukumu baina ya viongozi
wa Wilaya na Halmashauri.
“Nafahamu baadhi viongozi
mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa mnafahamu vizuri utendaji kazi
wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa kwa kipindi chote
kutenda kwa kadiri ya maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo
mbalimbali iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora ukiachilia
mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaina na kuyashuhudia katika
baadhi ya maeneo” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa “kupitia mafunzo
haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa
kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu
vyema Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka
na mgawanyo wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na
maadili ya viongozi wa Umma”.
Aidha Mhe. Jafo aliwataka viongozi
hao kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza mapambano
dhidi ya Dawa la kulevya, kulinda amani na utulivu katika maeneo yao
huku wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya Fedha za Serikali na
kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa
mapato ya Serikali.
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika
mafunzo hayo Naibu Katibu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu
Chaula amesema kitu cha msingi kati yetu sisi watendaji ni umoja ambao
kupitia huo utatuleta Ushindi na muongozo wa utendaji wetu uko kwenye
ilani ya Chama cha Mapindui hivyo kila mmoja wetu arejee Ilani ile ili
afahamu nini anachotakiwa kukifanya katika kipindi hiki cha miaka
mitano.
Awali akitoa taarifa ya
utangulizi kwa mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema mafunzo haya
yanatolewa na wataalamu walioboea katika masuala ya uongozi na
yatafanyika kwa muda wa siku tano kwa viongozi aidi ya 72.
Aliongeza kuwa maeneo ambayo
yatajen gewa uwezo ni namna bora ya kufanya maamuzi ya kimkakati
yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya Taifa, namna bora ya
kuongoza watu na kusimamia Rasilimali za Taifa na pia jinsi ya
kujijengea Sifa za kiungozi ambazo zinaleta heshima kwa jamii,
kuaminika na kutegemwa katika kuleta mabadiliko.
Mafunzo haya yamepangwa kufanyika
katika awamu nne(4) ambapo awamu mbili tayari zimekwsihafanyika
ziliojumuisha Wah. Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa kumi na
mbili(12) ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera,
Mwana, Mara, Simiyu, Geita na Manyara.
Awamu ya kwanzaya mafunzo haya ya
Uongozi yalifanyika Mwezi Mei, 2017 na yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na awamu
ya mwisho inatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Disemba 2017.
0 comments:
Post a Comment