Kumekuwa na shutma nyengine za kimataifa
zinazokosoa sheria mpya iliopitishwa na bunge la Israel ambayo
inahalalisha maelfu ya makaazi ya Israel yaliojengwa katika ardhi ya
Palestina huko West Bank.
Maafisa wa Palestina wanasema kuwa hatua
hiyo inahalalisha wizi, huku afisa wa Umoja wa Mataifa akisema
itaathiri matumaini ya kupata amani katika eneo hilo.
- UN yainyooshea kidole Israel
- US 'yaishutumu' Israel kuhusu makaazi mapya
- Israel kujenga makaazi 3000 zaidi huko West Bank
- Trump abadili msimamo kuhusu makaazi ya Israel
- Donald Trump aiambia Israel ''kukaa imara''
- Netanyahu: Israel haitaheshimu azimio la UN
Marekani imesema kuwa haitatoa tamko lake hadi pale mswada huo utakapoangaziwa na mahakama za Israel, ambapo huenda ukapingwa.
Mkuu wa Sheria amesema kuwa ni kinyume na katiba na kwamba hatautetea katika mahakama ya juu.
Sheria hiyo itasimamia nyumba 4000 huku wamiliki wake wa Palestina wakifidiwa.
Ni hatua za hivi karibuni zinazounga mkono makaazi zaidi ya Israel katika ardhi ya Palestina tangu rais Trump achukue mamlaka.BBC
0 comments:
Post a Comment