Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini
Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya
kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki
ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya
Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza
nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya
Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali
alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal
Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) akielezea riba nafuu ambayo wananchi wengi hupendelea
kutoka katika Benki baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya
UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall, Ofsini kwake jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika
Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada
ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall
OfIsini kwake jijini Dr es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Benki ya ya Uarabuni, UBL imesema iko
tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha
Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za
ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake.
Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini
Dar es Salaam.
Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa
Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa
kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani
lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha
nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya ya
Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha
Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya
Kilimo ni jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa
Sekta hii mama bado inakabiliwa na changamoto nyingi.
Alisema dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni
kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na
uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze
kupiga hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria
kuwa nchi ya Viwanda.
Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola
katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye mikopo,
Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia
kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu
biashara ya maduka ya fedha za kigeni.
“Tumepiga hatua ya kufunga mashine za
kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona
kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili.
Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi
cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na itaimarisha matumizi ya
shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa ya wananchi kutokudai
risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni,”
Alisisitiza Dkt. Mpango.
Katika kuhitimisha majadiliano hayo
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza
ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa
kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.
0 comments:
Post a Comment