METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, November 7, 2016

Ujerumani yapendekeza wahamiaji kurudishwa Afrika

Italien Flüchtlinge Rettung Mittelmeer (picture alliance/dpa/ Italian Navy Press Office)
Wizara za mambo ya ndani ya Ujerumani inataka kuwazuwiya wahamiaji kutofika kabisa katika mwambao wa Ulaya ulioko katika bahari ya Mediterenia kwa kuwachukuwa baharini na kuwarudisha Afrika.

Kwa kile kitakachokuwa mabadiliko makubwa kwa nchi hiyo yenye sera za ukarimu mkubwa wa kuomba hifadhi wizara hiyo imesema Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na sera kama ile ya Australia ambapo kwayo wahamiaji wanaodukizwa baharini wanapelekwa katika makambi yalioko katika nchi nyengine kushughulikia mchakato wao wa kuomba hifadhi.

Gazeti la Ujerumani la "Welt am Sonntag" limeripoti Jumapili (06.11.2016 )likimkariri msemaji wa wizara hiyo akisema kufuta uwezekano wa kufika Ulaya kunaweza kukawashawishi wahamiaji kuepuka kufunga safari zenye kuhatarisha maisha yao na zenze gharama kubwa.

Kwa mujibu wa wizara hiyo lengo lazima liwe kuwaondolea sababu makundi yanayosafirisha watu kwa magendo na kunusuru maisha ya wahamiaji kutokana na safari hizo za hatari.

Wizara hiyo inapendekeza wahamiaji wanaochukuliwa katika bahari ya Mediterenia ambao takriban wote wameondokea kutoka nchi iliyokumbwa na mzozo ya Libya wapelekwe Tunisia,Misri au mataifa mengine ya Afrika kaskazini kuomba hifadhi Ulaya kutokea nchi hizo.

Hifadhi iombwe nje

Iwapo maombi yao ya kuomba hifadhi yatakubaliwa hapo tena wahamiaji wanaweza kusafishwa kwa usalama kwenda Ulaya.

Wizara hiyo inaongozwa na Thomas de Madziere mwanachama wa cha Christian Demokratik cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambaye amekuwa akikosolewa kwa sera yake ya kuwafungulia milango wahamiaji ambapo chama hicho kimekuja kupoteza kura kwa Chama Mbadala kwa Ujerumani AfD katika uchaguzi wa majimbo wa hivi karibuni.

Wizara hiyo inasema pendekezo hilo liko katika hatua ya mwanzo na kwamba hakuna mpango madhubuti juu ya pendekezo hilo au mazungumzo katika ngazi ya Ulaya lakini wanasiasa wa upinzani wamelaani pendekezo hilo.

Bernnd Riexinger kiongozi wa chama cha upinzani cha sera za mrengo wa kushoto cha Die Linke amesema itakuwa ni kashfa ya kibinaadamu na hatua nyengine zaidi ya kufuta haki ya kupatiwa hifadhi.

Amesema maombi ya kuomba hifadhi yanapaswa yajazwe Ujerumani ili kuhakikisha waombaji wanapatiwa msaada wa kisheria na ameuita mfumo wa Australia kuwashughulikia wahamiaji haukubaliki kabisa.

Wahamiaji waendelea kuwasili

Askari wa mwambao wa Italia amesema hapo Jumamosi zaidi ya wahamiaji 2,200 wameokolewa kwa siku hiyo moja katika bahari ya Mediterenia na miili kumi ilipatikana.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limesema wiki iliopita kwamba watu 159,496 walifika Italia kwa njia ya bahari mwaka huu na 4,220 walikufa wakijaribu kuingia Ulaya kwa njia hiyo hilo likiwa ni ongezeko la watu 3,777 kwa mwaka mzima wa 2015.

Wengi waliohatarisha maisha yao kwa kuvuka bahari hiyo mara nyingi wanakuwa katika maboti yaliofurika yanayoendeshwa na makundi yanayosafirisha watu kwa magendo ambao wanakimbia mizozo na ukandamizaji kutoka kwenye nchi zao.DW
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com