Raia
wanne wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea katika
mji wa Bangui ambapo mashirika ya kiraia nchini Jamhuri ya Afrika ya
Kati yalikua yalitoa wito wa kusalia nyumbani kwa ajili ya kuomba
kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo.
Kikosi
cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kinashtumiwa
kushindwa kuyazima au kuyadhibiti makundi ya watu wenye silaha.
"Askari
wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca)
waliingilia kati mapema Jumatatu hii katika mji wa Bangui ili kuondoa
vizuizi vilivyokua vimewekwa barabarani na waandamanaji wanaowapinga,"
Minusca imebaini katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu hii jioni.
"Minusca
inalaani kabisa matukio ambayo yaliathiri baadhi ya maeneo ya mji mkuu
na inasikitishwa kuona hali hiyo imesababisha vifo vya raia wanne na
kuwajeruhi wengine 14, ikiwa ni pamoja na askari watano wa kikosi cha
Umoja wa Mataifa, " taarifa hiyo imeongeza. Vurugu hizi "ni jaribio mpya
la maadui wa amani kwa lengo la kuvuruga kurejea kwa hali ya kawaida ya
kikatiba."
Minusca
"pia inafutilia mbali kampeni ya kupakwa matope dhidi askari wa Umoja wa
Mataifa wa kulinda amani na itaendelea na kazi yake nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati. Minusca pia inakumbusha kwamba vurugu zozote zile dhidi
ya askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani zitapelekea wahusika
kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa," taarifa hiyo
imehitimisha.
RFI
0 comments:
Post a Comment