Waziri wa
mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Balozi Dkt. Augustine
Mahiga amesema ushirikiano wa Tanzania na umoja wa mataifa (UN)
wataendeleza ulinzi wa amani katika mataifa mbalimbali kama wanavofanya
kwa Sudan ya kusini.
Akizungumza
katika hafla ya miaka 71 ya umoja huo Dar es salaam , Balozi Mahiga
amewataka Vijana nchini kuchangamkie fursa za ajira zinazopatikana umoja
huo.hafla za miaka 71 za umoja wa mataifa zimehudhuliwa na viongozi
mbalimbali wa kitaifa na kimataifa huku suala la ulinzi ' pamoja na
amani likiwa limepewa kipaumbele kwa mataifa
Naye
Mwakilishi wa Mashirika wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amezitaja
changamoto zinazoikabili UN ni ongezeko la vijana ambapo wengi huwa
wanashindwa kuendana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kutokana na
miundombinu ya Elimu kutokuwa Rafiki.
Rodriguez
ameongeza kuwa Ili kuhakikisha UN inakabiliana na Changamoto hiyo
wameweka nguvu zaidi katika kuboresha Miundombinu ya Elimu barani Afrika
ili vijana kuweza kuendana na kasi ya utandawazi ili kuweza kujiajiri.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi
Augustine Mahiga akizungumza kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja wa
mataifa (UN) jana jinini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza kwenye hafla ya miaka 71 ya umoja mataifa (UN) jana jinini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment