Mbunge
wa Mkuranga, Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kukagua jengo
linalotarajiwa kuwa shule mpya katika kitongoji cha kikonda katika ziara
yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuru wananchi kwa kumchagua pamoja
kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani.
Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi katika kitongoji cha
Kikonda akiwa katika ziara yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu
wananchi kwa kumchagua pamoja na kuangalia maendeleo leo katika Kijiji
cha Bupa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza katika mkutano wa wananchi wa
kitogoji cha Kikonda juu ya changamoto zinazowakabili akiwa katika ziara
yake ya kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi kwa kumchagua pamoja
kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega akiwaonyesha wananchi Diwani wao,Abbas
Msangule jinsi ya kushirikiana naye kwa maendeleo katika Kijiji cha
Kondo Mwelazi katika ziara yake kijiji kwa kijiji kwa kushukuu wananchi
kwa kumchagua pamoja kuangalia maendeleo leo katika Kijiji cha Bupa
Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa
shule ya msingi Kondo Mwelazi alipowatembelea kujua mazingira walionayo
na kuwashukuru kuendelea na moyo licha ya kuwa na mazingira mgaumu leo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii -Mkuranga
Hayo ameyasema leo katika katika ziara ya vijiji vya kata ya bupu, Ulega amesema kuwa wakati umefika kwa kabila yake kusomesha watoto kwa ajili ya maendeleo kutokana dunia ya sasa inahitaji watalaam.
Ulega amesema kuwa changamoto zilizo katika kata ya Bupu ni maji pamoja na miundombinu ya barabara hivyo vinatakiwa kupatiwa ufumbuzi ili wananchi waondokane na changamoto hizo.
Mbunge huyo ameahidi kutoa Bati 50 katika shule mpya inayojengwa katika kitongoji cha kikonga kutokana watoto wa kitongoji hicho wanatembea kilomita sita. Ulega amesema changamoto zilizopo wilaya ya mkuranga zinatakiwa zitatuliwe kutokana na kuomba kazi ya kuwatumikia wananchi.
Amesema kuwa suala mfuko wa afya ya jamii CHF dawa hazipatikani na kufanya wananchi wengine washindwe kujiunga. Aidha amesema wananchi waliojiunga na CHF ni 65 ikiwa nia serikali ni watu wote wajiunge ili wasipate adha ya kupata huduma za afya.
Hata hivyo amesema nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona wananchi wanafurahia huduma zinazotolewa na serikali na sio vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment