JESHI la Polisi Mkoa wa Temeke limeua watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto alisema tukio hilo ni
la Oktoba 21 baada ya polisi kupata taarifa za kuwepo kwa kundi la watu
wanaodhaniwa ni majambazi.
Alisema baada ya taarifa, kikosi kazi cha Polisi cha Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, kilifanya ufuatiliaji na kubaini nyumba ambayo
haijakamilika imezungushiwa uzio na muda wote mlango wa uzio huo ulikuwa
umefungwa.
Aliongeza kuwa uchunguzi wa kina, ulifanyika na kubaini kuwa kweli
kundi hilo, lipo ndani ya nyumba hiyo na kwamba muda mwingi mlango wa
uzio, hufungwa na kuongeza kuwa majira ya saa tano askari wa kikosi kazi
cha mkoa huo na mkoa wa Pwani, kilizingira nyumba hiyo.
“Baada ya kujipanga mlango wa uzio huo uligongwa na kutoa amri ya
kuwataka walioko ndani ya nyumba hiyo wafungue mlango na kujisalimisha,
lakini tulishangaa baada ya amri hiyo ghafla milio ya risasi ilianza
kutoka ndani ya nyumba hiyo,” alisema Muroto.
Aliongeza kuwa baada ya milio hiyo, askari ambao walikuwa makini na
wakiwa wamezingira nyumba hiyo wakiwa wamejipanga katika miundo ya
mapigano, walianza mashambulizi kujibu mashambulio hayo.
Alisema majibizano yaliendelea na watu hao waliokuwa wanashambulia
kutoka ndani, walivunja uzio na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watano
walitoka huku wakiwa wanashambulia.
Muroto alisema askari waliendelea kupambana nao na kufanikiwa
kuwajeruhi baadhi yao, na wengine walifanikiwa kutoroka na silaha zao.
“Mashambulizi kutoka ndani yalitulia na askari waliingia ndani ya
uzio, kwa kuwa yalikuwa mapambano ya nguvu walikuta majambazi watatu
wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 na 30 wakiwa wamejeruhiwa
kwa risasi na hali zao zilikuwa mbaya na tuliwapeleka Hospitali ya Taifa
Muhimbili lakini walibainika kuwa tayari wameshakufa na miili yao
imehifadhiwa hapo ikisubiri kutambuliwa,” alisema.
Alisema baada ya kufanya upekuzi, polisi walikuta silaha moja aina ya
short gun pump action yenye MV.51516 R na namba ya usajili TZ car 99987
na risasi tano ndani ya magazini yake.
Risasi nyingine sita za short gun zilikutwa ndani ya mfuko wa plastiki pamoja na risasi nane za pistol.
Aidha alisema katika tukio hili, ilibainika kuwa kuna askari mmoja
alijeruhiwa bega lake la kushoto na lilikuwa jeraha kubwa la risasi,
hivyo alipelekwa katika Hospitali ya Muhimbili ambako amelazwa na
anaendelea kupata matibabu akisubiri kufanyiwa upasuaji.
Muroto alisema ufuatiliaji wa majambazi, walitoroka eneo la mapambano
uliendelea kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mtambani, ambapo
majira ya saa tatu asubuhi jambazi mmoja alipatikana akiwa mahututi na
juhudi za kumfikisha hospitali zilifanyika. Hata hivyo, alikufa akiwa
njiani.
”Tunawashukuru wananchi wote wema kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha
kwa Jeshi la Polisi, kwa kuliunga mkono katika kufichua wahalifu na
kupambana na wahalifu, nitoe tahadhari kuwa mkoa huu ukifanya tukio ujue
utashughulikiwa kabla hujakamilisha na ukifanikiwa kukamilisha azma
yako haitachukua muda utakamatwa,” alisisitiza.
Saturday, October 22, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment