Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustine Kamuzora
akiwa na mwakilishi kutoka Benki ya Dunia anaeshughulikia masuala ya
Habari na Mawasiliano Bi.Boutheina Guermazi wakati wa warsha ya Habari
na Mawasiliano ikizungumzia mafanikio ya mradi wa kuboresha miundombinu
ya Mawasiliano nchini na Serikali mtandao.
Na Daudi Manongi, MAELEZO
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora
amesema kuwa kata 345 zimefaidika na mradi wa kuboresha miundombinu ya
mawasiliano nchini na Serikali mtandao kupitia mfuko wa mawasiliano kwa
wote.
Profesa
Kamuzora amesema hayo katika Warsha ya Habari na Mawasiliano
iliyoandaliwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na Wizara hiyo
ikizungumzia mafanikio ya mradi wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano
nchini na Serikali mtandao.
“Kupitia
Serikali mtandao tunataka huduma za serikali ziwafikie wananchi kokote
walipo na tunafahamu sasaivi wananchi wengi wana simu za mkononi na
hivyo tunataka huduma kama za manunuzi kama tenda za Serikali na usajili
wa vizazi na vifo kuanzia sasa zipatikane kwa njia ya mtandao ,huduma
hii itaongeza uwazi,ufanisi na ubora wa huduma katika shughuli
mbalimbali za Serikali.”Alisema Prof Kamuzora.
Pia
Profesa Kamuzora amesema kuwa Mradi huo ulilenga kufikisha mawasiliano
vijijini na maeneo ambayo ni magumu kufikika na wafanyabiashara na
ilipata mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 100 kutoka Benki ya
Dunia ambao umesaidia kutoa ruzuku kwa makampuni mbalimbali ya simu ili
yaweze kujenga minara kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara na
hivyo kufanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2.
Kwa
upande wake Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia anaeshughulikia masuala ya
Habari na Mawasiliano Bi.Boutheina Guermazi amesema kuwa wataendelea
kusaidia sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwa ni muhimu katika maendeleo
ya nchi yeyote na hivyo hawatasita kutoa misaada mbalimbali iwapo
watahitajika kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment