Accra, mji mkuu wa Ghana, ambapo Ibrahim Mahama, ndugu wa rais John MAhama alipoendesha mkutano wa kisiasa.
Jeshi la
Ghana limechukua hatua za kinidhamu kwa askari ambao walitoa ulinzi kwa
Ibrahim Mahama, ndugu wa Rais John Mahama, wakati wa mkutano wa kisiasa
uliyofanyika Jumapili iliyopita.
Askari hawakuwa waliruhusiwa kutoa ulinzi kwa mfanyabiashara, kwa mujibu wa Kanali Aggrey Quashie, msemaji wa jeshi la Ghana.
Askari
walitoa ulinzi kwa msafara wa Ibrahim Mahama ni sehemu ya kikosi cha
askari wanaolinda taasisi za nchi na hawakupata maelekezo ya kuwa katika
ulinzi wa ndugu wa rais wa nchi, kanali Quashie amesema.
jeshi
limeanzisha uchunguzi kuhusu askari hao, kufuatia picha za
mfanyabiashara Ibrahim Mahama zilizorushwa ambapo aanaonekana
akizungukwa na "watu kadhaa wenye silaha za kivita, watu ambao walikua
wamejidhatiti, " imeandikwa katika ukurasa wa Facebook wa radio ya taifa
ya Ghana.
Shahidi
mmoja amerusha ujumbe katika ukurasa wa Facebook, akidai kuwa kulikua
pia na magari ya kivita katika ulinzi wa ndugu wa rais Mahama.
RFI
0 comments:
Post a Comment