MKURUGENZI Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoa wa
Tanga, Emmanuel Mkumbo (41) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumtishia kumuua kwa bastola
askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani hapa na kuvunja sheria
za usalama barabarani.
Mkumbo ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam, alipandishwa
kizimbani jana na alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Agripinas
Kimanze kutoka kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Sunday Hyera,
akisaidiana na Ediga Bantulaki.
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa serikali, mshitakiwa huyo
anakabiliwa na kesi mbili, ya kwanza ikiwa ni kesi ya jinai kwa mujibu
wa Kifungu cha 226 ya mwaka 2016 na ya pili ni kesi ya Usalama
Barabarani kwa mujibu wa Kifungu cha 222.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, mwaka huu eneo
la Mkambarani wilaya ya Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es
Salaam wakati akiendesha gari aina ya Toyota Pajero lenye namba za
usajili T 845 CTJ.
Kosa la kwanza linalomkabili Mkurugenzi Mtendaji huyo ni kujaribu
kumtishia kumuua kwa bastola askari aliyejulikana kwa jina la Koplo
Titunda, akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Makosa mengine ni kuendesha gari lenye namba T845 CTJ aina ya Toyota Pajero bila ya kuwa na leseni na kuendesha gari bila bima.
Hyera alidai kuwa makosa mengine ni mwendo kasi katika eneo
lililoruhusiwa kuendesha mwendo wa spidi 50 kwa saa lakini alivuka na
kufikia 85, kugoma kupeleka gari kituo cha Polisi na kuendesha bila
uangalifu barabarani.
Mshitakiwa huyo alikana makosa hayo na kuachiwa kwa dhamana, huku
kesi yake ikitarajiwa kufikishwa tena mahakamani Oktoba 31, mwaka huu.
Hata hivyo, jitihada za waandishi wa habari kupata picha halisi ya
mtuhumiwa, hazikufanikiwa baada ya askari kumziba mtuhumiwa kwa koti
pamoja na kofia aina ya pama na kumuingiza katika gari aina ya Toyota na
kuondoka.
Monday, October 17, 2016
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Richmond Raymond akipokewa na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mwanza baada ya kuwasili na tuzo za ushindi akitokea nchini Afrika ya Kusin...
-
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi kijijini Ipanko Wilaya ya Ulanga wakati wa ziara ya kikazi ya siku...
-
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka watanzania kutumia fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashari...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment