Pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba ya Zuma zilikuwa ni za mlipa kodi
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi jinsi ilivyoamriswa na mahakama.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anaripoti kuwa msemaji wa wizara ya fedha amethibitisha kuwa pesa hizo zimepokelewa.
Wizara ya
fedha nchini Afrika Kusini ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma
alihitajika kurejesha dola 509,000 kwa serikali, pesa zilizotumiwa
kukarabati nyumba yake huko Nkandla.
Makao ya binafsi ya Zuma ya Nkandla
Mahakama
ya juu zaidi nchini humo ilikuwa imetoa uamuzi mapema mwaka huu, kuwa
Zuma alipe dola milioni 23 pesa za umma zizotumiwa kwa nyumba yake mwaka
2009.
Sakata ya Nkandla ilitishia wadhifa wake Zuma. Alikwepa hatua ya kumuondoa madarakani na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Hata hivyo aliomba msamaha kwa njia ya runinga mwezi Aprili akisema kuwa suala hilo limeleta aibu.
BBC
0 comments:
Post a Comment