METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, September 11, 2016

WAZIRI WA MAENDELEO YA MIJI NA VIJIJI WA NAMIBIA AFIKA NCHINI KUJIFUNZA UTAWALA WA ARDHI

ang1
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa amewasili Ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, akiwa ameambatana na ujumbe wake, uliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.

ang2
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akielekezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Mb). na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje kutumia kwa ajili ya kupata huduma katika Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.
ang3
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa ameambatana na ujumbe wake ndani ya Kituo cha Huduma kwa Mteja – Wizarani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje, akipewa maelekezo na mtumishi jinsi huduma zinavyotolewa katika Kituo hicho. Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.
ang4
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akikabidhi Dola 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora  katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Waziri huyo amefika nchini na ujumbe wake kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
ang5
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa kijiji hicho kuwa mfano bora  katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi bora ya Ardhi. Katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Sekta ya Ardhi na ujumbe ulioambatana na Waziri kufika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
ang6
Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ; Angeline Mabula, kushoto kwake. Kulia kwake ni Kaimu Kamishna wa Ardhi ; Mary Makondo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje pamoja na wajumbe walioambatana na Waziri huyo wa Namibia, waliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.

Waziri wa Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa amefika nchini na ujumbe wa Wataalamu wake kwa ajili ya kujifunza taratibu za Utawala wa Ardhi wa Tanzania.

Waziri huyo alianza ziara yake fupi ya kujifunza Utawala wa Ardhi kwa kuonana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi ofisini kwake akiwa ameambatana na ujumbe wake.

Waziri ameeleza kuwa Bunge nchini Namibia limewaelekeza kufika Tanzania kujifunza taratibu zinazofanywa katika eneo la Utawala wa Ardhi, baada ya Bunge hilo kuona mfano mzuri wa nchi ya Tanzania kati ya nchi nyingine za Afrika walizofanyia tathimini katika eneo hilo.

Katika ziara yake, Waziri huyo amejifunza Huduma zinazotolewa katika Kituo cha Huduma kwa Mteja Wizarani, kutembelea wilaya ya Kisarawe, katika kijiji cha Kurui ambapo eneo hilo ni mfano bora wa Utekelezaji wa Mpango wa Matumizi bora ya Ardhi, kutembelea ofisi za Programu ya kuwezesha umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP) na Kituo cha Uwekezaji(Tanzania Investment Company – TIC).

Aidha, Waziri huyo ameeleza kuwa amenufaika sana kwa kujifunza mengi mazuri, na amependa zaidi utaratibu mzuri uliopo katika eneo la uwekezaji wa ardhi, na kusema kuwa atafanyia kazi yale aliyojifunza.

Waziri alipokuwa akitoa shukrani zake wakati anaaga katika ofisi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Mb). Mhe. Mabula alisema amefarijika kuona kuwa jopo hilo limeona mazuri yaliyomo ndani ya Utawala wa Ardhi nchini Tanzania. Aliendelea kusema; “ Sekta ya Ardhi bado ina changamoto nyingi, hasa ile ya Migogoro iliyopo kati ya Wakulima na Wafugaji, hatahivyo Wizara inajitahidi kuendelea kukabiliana na changamoto hiyo”.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com