Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa
amewasili Ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. William Lukuvi, akiwa ameambatana na ujumbe wake, uliofika nchini
kujifunza kuhusu Utawala wa Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akielekezwa na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula
(Mb). na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji,
Immaculate Senje kutumia kwa ajili ya kupata huduma katika Kituo cha
Huduma kwa Mteja – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri huyo amefika nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akiwa
ameambatana na ujumbe wake ndani ya Kituo cha Huduma kwa Mteja –
Wizarani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje, akipewa maelekezo na mtumishi
jinsi huduma zinavyotolewa katika Kituo hicho. Waziri huyo amefika
nchini kujifunza Utawala wa Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akikabidhi
Dola 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa
kijiji hicho kuwa mfano bora katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi
bora ya Ardhi. Waziri huyo amefika nchini na ujumbe wake kujifunza
kuhusu Utawala wa Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa akimpa mkono
wa pongezi Mwenyekiti wa kijiji cha Kurui – Kisarawe, kama pongezi kwa
kijiji hicho kuwa mfano bora katika Mpango wa Utekelezaji wa Matumizi
bora ya Ardhi. Katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Sekta
ya Ardhi na ujumbe ulioambatana na Waziri kufika nchini kujifunza kuhusu
Utawala wa Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa, katikati
akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ; Angeline Mabula, kushoto kwake. Kulia kwake ni
Kaimu Kamishna wa Ardhi ; Mary Makondo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Mipango Miji na Vijiji, Immaculate Senje pamoja na wajumbe walioambatana
na Waziri huyo wa Namibia, waliofika nchini kujifunza kuhusu Utawala wa
Ardhi.
Waziri wa
Maendeleo ya Miji na Vijiji wa Namibia; Sophia Shaningwa amefika nchini
na ujumbe wa Wataalamu wake kwa ajili ya kujifunza taratibu za Utawala
wa Ardhi wa Tanzania.
Waziri
huyo alianza ziara yake fupi ya kujifunza Utawala wa Ardhi kwa kuonana
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi
ofisini kwake akiwa ameambatana na ujumbe wake.
Waziri
ameeleza kuwa Bunge nchini Namibia limewaelekeza kufika Tanzania
kujifunza taratibu zinazofanywa katika eneo la Utawala wa Ardhi, baada
ya Bunge hilo kuona mfano mzuri wa nchi ya Tanzania kati ya nchi
nyingine za Afrika walizofanyia tathimini katika eneo hilo.
Katika
ziara yake, Waziri huyo amejifunza Huduma zinazotolewa katika Kituo cha
Huduma kwa Mteja Wizarani, kutembelea wilaya ya Kisarawe, katika kijiji
cha Kurui ambapo eneo hilo ni mfano bora wa Utekelezaji wa Mpango wa
Matumizi bora ya Ardhi, kutembelea ofisi za Programu ya kuwezesha
umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP) na Kituo cha
Uwekezaji(Tanzania Investment Company – TIC).
Aidha,
Waziri huyo ameeleza kuwa amenufaika sana kwa kujifunza mengi mazuri, na
amependa zaidi utaratibu mzuri uliopo katika eneo la uwekezaji wa
ardhi, na kusema kuwa atafanyia kazi yale aliyojifunza.
No comments:
Post a Comment