Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili
kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel
Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa pili kushoto) wakati akiwasili katika
Uwanja wa Karume kuhitimisha mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka
17 ya Airtel Rising Star Septemba 11, 2016 kushoto ni Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Jamali Malinzi.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na
wanamichezo, wadau wa michezo na wanahabari kabla ya kushuhudia fainali
ya mashindano hayo yiliyohitimisha mashindano hayo kwa Vijana chini ya
umri wa miaka 17 Airtel Rising Star katika Uwanja wa Karume Jijini Dar
es Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua
wachezaji wa timu ya Morogoro Boys kabla ya kuanza kwa fainali kati yao
na timu ya Ilala iliyofanyika katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es
Salaam Septemba 11, 2016.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikabidhi
kikombe kwa nahodha wa Timu ya wasichana ya Temeke walioibuka washindi
wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Star
kwa upande wa wasichana katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam
Septemba 11, 2016.
0 comments:
Post a Comment