Mmoja wa wakurugenzi wateule Bw.Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Wakurugenzi
wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa siku ya
Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti
vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.
Zoezi la
uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya
Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.
Wakurugenzi
hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa mmoja,
Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11,
wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00
asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016
inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya
vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa
umma.
Taarifa
hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa
lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa
kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.
Wakurugenzi
hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa
Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank
Bahati Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na
Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
0 comments:
Post a Comment