Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamesababisha watu wengi kuhama makwao
Umoja wa
Mataifa unasema kuwa idadi ya watu waliokimbia nchi ya Sudan Kusini
kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo imepita watu
milioni moja.
Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya watu 185,000 ambao wameikimbia nchi kufuatia mapigano mapya yaliyoanza mwezi Julai.
Zaidi ya watu milioni 1.6 nao wamelazimika kuhama makwao ndani ya Sudan Kusini.
Mapigano yaliyozuka mwaka 2013 yameendelea hadi sasa
Kati ya
hao wakimbizi 373,626 wameingia nchini Uganga huku theluthi moja kati
yao wakiwasili tangu mwezi Julai na 20,000 wiki iliyopita. Wale
wanaowasili sasa wanasema kuwa kuna mapigano mapya huku raia
wakishambuliwa na makundi yaliyojihami ambayo hupora, huwadhulumu
kimapenzi wanawake na wasichana na kuwaingiza jeshini vijana wa kiume.
Wakimbizi
292,000 waliingia nchini Ethiopia huku 11,000 wakivuka na kungia
Gambella wiki iliyopita. Wale wanaowsili kwa sasa wanatoka jamii ya Nuer
wakiwemo watoto 500 wasioandana na wazazi.
Watu 185,000 wameikimbia nchi kufuatia mapigano mapya yaliyoanza mwezi Julai
247,317 wamewasili nchini Sudan, 1800 wakiwasili kila mwezi katika jimbo la White Nile na mafuriko yakiwazuia wengine.
Nchini
Kenya wakimbizi 90,000 wamewasili nao wengine 300 wanawasili kila wiki
kutokana na sababu za kiusalama, uchumi mbaya na ukame.
Wakimbizi 40,000 wamesili nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo katika mkoa wa Ituri.
Tofauti kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar zilisababisha kuzuka kwa vita
Wakimbizi
wengi wanoawasili nchini Uganda ambayo inawapa makao wakimbizi wengi
kutoka Sudan Kusini, wanaonekana wamechoka baada ya kutembea siku kadha
msituni bila chakula wala maji.
Tofauti
kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar
zilisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi
Disemba mwaka 2013.
Makadirio
ya idadi ya watu nchini Sudan Kusini ni kati ya watu milioni 10 hadi
milioni 12. Hii inamaaanisha kuwa takriban asilimia 20 ya watu hao
hawana makao kutokana na mzozo uliopo. BBC
0 comments:
Post a Comment