Mkuu wa
kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga
akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya uhamasishaji katika Wiki
ya Nenda kwa Usalama barabarani kutoka kampuni ya TBL Group,katikati ni
Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter na kushoto ni Mkurugenzi
wa huduma za Zahanati Mwendo,Rosemary Mwakitwange.
Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter,akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga
akimpongeza Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter baada ya
kutembelea gari la kupima afya za madereva
Kamanda mpinga akipokea baadhi ya vifaa vya uhamasishaji usalama vilivyotolewa na TBL Group
Kamanda mpinga akipokea baadhi ya vifaa vya uhamasishaji usalama vilivyotolewa na TBL Group
Katika
jitihada za kutokomeza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group
jana imetoa vifaa vya uhamasishaji wa usalama katika wiki ya Nenda kwa
Usalama barabarani vilevile imekuja na huduma mpya ya kupima afya za
madereva ya zahanati inayotembea ‘Zahanati Mwendo’.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,Afisa Mawasiliano wa TBL
Group,Amanda Walter,alisema kuwa msaada huu ni mwendelezo wa kampuni
kushiriki katika kampeni za Usalama barabarani.
“TBL
Group ikiwa ni kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kwa muda
mrefu tumekuwa tukifanya kazi na serikali kupitia Jeshi la polisi katika
kampeni za kuhamasisha usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni
kutokomeza matukio ya ajali nchini kupitia kampeni yetu ya usalama na
Unywaji wa Kistaarabu”.Alisema Amanda.
Alivitaja
vifaa vya uhamasishaji usalama katika Wiki ya Nenda na Usalama
Barabarani kuwa ni Stika 1,000,Tisheti 1000 na kofia 500 na imewezesha
upimaji wa afya za madereva kupitia Zahanati Mwendo “Huduma hii ni gari
maalumu lenye vifaa vya kupima afya za madereva na wataalamu wa afya na
litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kupima afya
za madereva na kuwapatia matibabu na huduma hii itakuwa inapatikana bure
kuanzia sasa hadi mwanzoni mwa mwezi ujao na tutaendelea kufanya
kampeni zaidi”.Alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la
Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga ,kwa niaba ya serikali aliishukuru TBL
Group na wadau wengine ambao wanashirikiana na jeshi hilo kufanikisha
kampeni za usalama barabarani.
Alisema
bado kuna matukio mengi ya ajali nchini ambazo zinasababisha vifo vya
watu wengi na kuleta hasara nyingi hivyo kunatakiwa jitihada za pamoja
kufanya kampeni ya kuzipunguza ikiwezekana hata kuzimaliza kabisa.
“Mwaka
huu TBL Group wamekuja na huduma ya kupima afya za madereva kupitia
Zahanati inayotembea ambayo ni ya aina yake nchini hivyo natoa wito kwa
madereva wote watakapoona gari hili maalumu litakalozunguka sehemu
mbalimbali wajitokeze kupima afya zao na kutakuwepo na vipimo vya
macho,shinikizo la damu ,sukari na vinginevyo tena vinatolewa
bure”.Alisema Kamanda Mpinga.
0 comments:
Post a Comment