Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando
Na. Abushehe Nondo & Frank Shija
JUMLA ya
kaya 26,248 zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III)
kwa kupatiwa jumla ya shilingi Bilioni 6.6 katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mmbando
amesema kuwa utambuzi wa kaya maskini ulianza mwezi Januari 2015 kwa
kushirikisha wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo jumla ya kaya
26,248 zilizoandikishwa na kupokea ruzuku kila baada ya miezi miwili
kwa kuzingatia mzunguko wa malipo.
Aliongeza
kuwa wanufaika wa mpango huo wamepatikana kutokana na ushirikishwaji wa
jamii husika ambapo jamii yenyewe ilibainisha majina ya walengwa katika
maeneo yao.
Aidha
Mmbando amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo kuna baadhi ya changamoto
zilizojitokeza katika kutekeleza mpango huo ikiwemo baadhi ya kaya
zilizokidhi vigezo kukataa kuandikishwa, kuandikishwa kwa kaya
zisizokuwa na sifa, pamoja na kupokea ruzuku pungufu.
Katika
kukabiliana na changamoto hizo, Mmbando amesema mpaka sasa jumla ya kaya
609 zimeondolewa katika kwenye mpango huo ikiwemo kaya 141 (Ilala),
kaya 296 (Kinondoni) na kaya 172 (Temeke).
Kwa
upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Dar es Salaam, Esterine Sephania
amesema kuwa suala la udanganyifu wa kuandikishwa kwa walengwa wasiokuwa
na sifa linaanzia katika ngazi ya serikali za mitaa ambapo huko ndiko
wanaleta majina.
0 comments:
Post a Comment