METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 14, 2016

Rais wa zamani Brazil na mkewe wafunguliwa mashitaka ya rushwa

Lula na mkewe
Lula na mkewe
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva,amefunguliwa mashtaka ya rushwa na wizi wa fedha, yeye pamoja na mke wake.
Mwendesha mashtaka wa seriakali Deltan Dallagnol amesema kuwa Lula alikua kinara wa rushwa na kashfa ya kampuni ya kickback inayomilikiwa na serikali, Petrobras ambayo ilikua na nia ya kuwaacha wafanyakazi wake serikalini.
Lula anashukiwa pia kukubali nyumba ya kifahari katika ufukwe wa Guaruja kutoka kwa kampuni ya ujenzi iliyopewa mkataba kipindi yeye yupo madarakani.
Wanasheria wa Rais huyo wa zamani wanasema kuwa hakuna ushahidi wowote wa madai hayo.
Upelelezi pia umehusisha nyumba za kifahari za kupangisha katika mwambao wa Guaruja
Upelelezi pia umehusisha nyumba za kifahari za kupangisha katika mwambao wa Guaruja
chini ya sheria ya Brazil hakimu ataamua kukubali au kukataa kupokea mashtaka hayo ndani ya siku zijazo. BBC
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com