METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, September 14, 2016

WADAU WAENDELEA KUJITOLEA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA


Na Faustine Ruta, Bukoba.

Mchungaji King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka Maeneo ya Kahororo Kyamaizi Bukoba, King James ambaye pia ni mmoja wa wadau wa maendeleo Manispaa ya Bukoba jana jumatano septemba 14, 2016 jioni amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni baada ya maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea jummosi iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka. 
King James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai, Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na nyumba zao kubomolewa.

Takribani shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa mkoani Kagera. 
Hamugembe Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi na Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi ya Wakazi 6.
Wengi mpaka sasa wanapikia nje baada ya nyumba zao kubomolewa.
Moja ya Nyumba iliyobomolewa na Tetemeko ndani ya Mtaa wa Hamugembe Omukishenye.
King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) Bukoba akiteta na Watoto Yatima katika Kituo hicho chenye makazi yake Hamugembe.
Bi. Saada akishukuru kwa Msaada aliopokea kutoka kwa King James ambao ni wa dharura kutokana na Tetemeko la Ardhi lililotokea hivi karibuni.
King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) akitoa Misaada ya Mchele katika kituo hicho cha Yatima ambacho ni kikongwe katika Mji huu wa Bukoba ambacho mpaka sasa kinalea watoto zaidi ya 36.
Mtoto mdogo zaidi anayelelewa katika kituo hicho cha yatima kilichopo Hamugembe ambaye ameokotwa hivi karibuni mwezi uliopita ambaye King James ameguswa nae.
King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) akiwa amebeba Mtoto Mchanga aliyeokotwa hivi karibuni na wapita njia na kumpeleka katika kituo hicho. Mchungaji James amehaidi kukisaidia kituo hicho kwa kukijengea Vyumba Viwili vya kulala.
Furaha kwa Mama Saada mama Mlezi wa Watoto Yatima baada ya kutembelewa na kupokea Misaada, Na hapa akiwashukuru wageni hao waliompatia msaada huo wa Dharura katika kipindi hiki kigumu kinachowalaza nje baada ya Nyumba yao kuangushwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Jumamosi septemba 10, 2016.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com