|
Maandalizi ya kumkaribisha waziri mkuu Kasim Majaliwa Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera Mjini Bukoba |
|
Wananchi
mbalimbali waliojitokeza kuungana pamoja kuwaaga waliopoteza maisha
kufutia tetemeko hilo wakiwa wameketi kitako wakimsubilia Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa kuwasili Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba Leo |
|
Wananchi wakisikiliza kwa makini kinachoendelea
|
|
Maandalizi yakiwa
bado yanafanyika kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuwaaga marehemu
waliopoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi la hapo jana |
|
Viongozi wakiwa
wamebeba mwili wa mmoja kati ya waliopoteza maisha kufuatia tetemeko
hilo tayari kwa kuagwa katika uwanja wa Kaitaba BUKOBA mjini |
|
PICHA ZOTE NA MWANAWAMAKONDA BLOG |
Waziri Mkuu
wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameungana na Wakazi wa bukoba leo Septemba 11,2016
kufuatia Tetemeko la ardhi la ukubwa wa
mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nchini na
kupelekea kuuawa kwa zaidi ya 10 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa huku majengo mengi
yakibomoka.
Tetemeko hilo hasa likileta matatizo makubwa mkoani Kagera kwa Wakazi wa
Manispaa ya Bukoba na Vitongoji vyake.
Katika
taarifa ya Ikulu jana, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salim Kijuu kutokana na vifo vya watu kadhaa
vilivyotokea kutokana na tetemeko hilo la ardhi katika maeneo mbalimbali ya
mkoa huo.
Katika
salamu hizo, Rais Magufuli ameeleza kushitushwa na taarifa za tukio hilo
lililosababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha, wengine kujeruhiwa pamoja
na uharibifu wa mali. Amesema anaungana na familia zote zilizopoteza ndugu,
jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe mahali pema peponi. Amina.
“Kupitia
kwako Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu na
wakuu wa mikoa jirani yako iliyokumbwa na tukio hilo, natoa pole kwa familia,
ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea kwa Mwenyezi
Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema
Rais Magufuli na kuwaombea wote walioumia katika tetemeko hilo wapone haraka.
0 comments:
Post a Comment