Na: Frank Shija, MAELEZO
MSAADA wa
Shilingi bilioni 6.3 umetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara
yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Ihungo iliyo haribika baada ya kuathiriwa na tetemeko la
Ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba mkoani Kagera.
Hayo
yabainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu huo.
Profesa
Ndalichako amesema kuwa msaada huo umetokana na ziara aliyoifanya tarehe
17 na 18 mkoani Kagera ambapo mwakilishi kutoka DFID nchini alishiriki
katika zaiara hiyo na kutembelea shule zilizo haribika kutoka na
tetemeko hilo.
“Baada ya
bunge kuisha tarehe 17 na 18 nilifanya ziara ya kutembelea shule
zilizoharibika kutokana na tetemeko, kwa bahati wadau wetu wa maendeleo
DFID waliungana name kutembelea shule za Ihungo na Rugambwa kutokana
ziara ile wameamua kutusaidia” Alisema Ndalichako.
Kufuatia
ziara hiyo ambapo walijionea uharibifu mkubwa wa majengo ya shule ya
Ihungo na nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa, DFID
waliguswa na athari walizozikuta na kuamua kusaidia ujenzi wa Shule ya
Ihungo na nyumba 10 za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Rugambwa.
Amesema
kuwa msaada huo umelenga kujenga upya shule ya Sekondari ya Ihungo ikiwa
ni pamoja na kujenga maabara ya kisasa na kununua samani
zilizoharibika.
Mpaka
sasa wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapo mkoani
Kagera mabapo leo wanakabidhiwa shule hizo na Manispaa ya Bukoba ili
waanze ujenzi wake unaotarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini (DFID
Tanzania) Vel Gnanendran amesema kuwa Serikali ya Uingereza imeguswa
sana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera.
“Kwa
niaba ya Serikali ya Uingereza tunatoa pole sana kwa Mhe. Rais Magufu na
waathirika wote wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kwa ni tukio lisilo
pangwa”. Alisema Mkuu huyo.
Vel
amesema kuwa lengo kubwa la wao kutoa msaada huo ni kuhakikisha
miundombinu ya shule zilizoharibika kujengwa haraka ili wanafunzi waweze
kurejea mashuleni katika wakiwa katika hali ya kawaida.
“Tumeguswa
sana na athari zilizotokana na tetemeko la Kagera, Serikali ya
Uingereza kupitia ofisi ya DFID Tanzania imetoa msaada wa pound milioni
2.23 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 6.3 za Kitanzania”. Alisema Vel.
0 comments:
Post a Comment