NA LEAH MUSHI
Chama cha
watanzania waliosoma China- CHINA ALLUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA
(CAAT) hii tarehe 27 Agosti, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa
ajili ya kupata viongozi wake wapya.
Uchaguzi
huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green views Hotel sinza
Dar es salaam kuanzia saa saba kamili mchana na kufuatiwa na sherehe ya
kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza muda wao.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho GUSTAV SANGA uchaguzi
huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba
ya chama hicho.
Nafasi
zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Chairperson, Secretary, Treasurer,
Director of Statistics, media and information, Director of Art, culture
and heritage pamoja na Director of Education, Science and Technology
SANGA pia
amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika chama
hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo
kuishauri serikali masuala yahusuyo TANZANIA- CHINA.
0 comments:
Post a Comment