Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka
huu jumla ya watanzania milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa
vitambulisho vya Uraia.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami amesema
kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
la kuitaka Mamlaka hiyo kuweka saini ya mwombaji na mtoaji wa
vitambulisho hivyo.
“Tumeanza
kutekeleza agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii
inamaanisha kwamba vitambulisho vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni
mpaka leo vina saini ya muombaji, saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa
muombaji” amefafanua Mdami.
Ameeleza
kuwa kazi ya ugawaji wa vitambulisho hivyo inasubiri kuzinduliwa na
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli atakayekabidhiwa kitambulisho cha
uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wananchi
wengine.
Mdami
amesema ifikapo Desemba 31 mwaka huu NIDA itakuwa imetoa namba za
utambulisho wa vitambulisho hivyo kwa watanzania milioni 23 kwa kutumia
taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika vitambulisho vya
kupigia kura na kuziamishia katika kanzi data ya NIDA.
Amefafanua
kuwa ili mwananchi aweze kupata kitambulisho cha uraia atalazimika
kufika katika ofisi za NIDA akiwa na vielelezo vinavyoonyesha mwaka wake
wa kuzaliwa pamoja uthibitisho wa uraia wake hii ni kutokana na NEC
kutokuwa na viambatanisho hivyo.
Amebainisha
kuwa mwananchi mwenye namba ya utambulisho anaweza kupata huduma zote
zinazohitaji namba ya kitambulisho cha Uraia kutokana na namba hiyo
kutobadirika na kuendelea kutumika hata baada ya kitambulisho
kuchapishwa.
Amesema
mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wamekwisha patiwa vitambulisho hivyo
na milioni 6.5 wamesajiriwa kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo.
Aidha,
Vitambulisho hivyo vya zamani vitaendelea kutumika mpaka
utakapotangazwa utaratibu wa kuvibadirisha kwa ajili ya kupata
vitambulisho vipya.
Pia
ametoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya watu wanaodai kwamba wa
kumekuwa na mlolongo mrefu wa kupata vitambulisho hivyo kwa kueleza
kuwa NIDA haina namna ya kufupisha mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni
sawa na kuuza uraia wa Tanzania.
Amesisitiza
kuwa ni lazima NIDA ijiridhishe juu ya uhalali na sifa za muombaji ni
kuwa ni Mtanzania kwa kuambatanisha vielelezo vinavyohitajika.
0 comments:
Post a Comment