Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu
Duniani (UNFPA) anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni Dk. Natalia
Kanem (wa pili kutoka kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati)
mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga jana jijini Dar es
salaam.Wengine alioambatana nao ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina
Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia)
akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya
Umoja yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania jana jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem
anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda
wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
(Mb.)akiangalia moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa
mwaka 2016 -2021 alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu
(katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza muda wake hapa nchini
Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na
Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa
katika picha ya pamoja huku wakionesha chapisho la lenye Mipango ya
Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 jana jijini Dar es salaam. Picha/Aron
Msigwa –MAELEZO.
Na. Mwandishi Wetu – Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia
kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu
usawa wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.
Amesema Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Tanzania.
Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika katika jamii ya watanzania
Aidha,amesema
kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama
wajawazito kwa kuweka miundombinu na mazingira bora ya
kujifungulia huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na
kuhamasisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa
mpango.
0 comments:
Post a Comment