Katibu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Siraji Madebe anayesalimiana na Rais Dk. John Pombe Magufuli
Shirikisho
la vyuo vya Elimu ya Juu CCM katika kikao chake cha kazi cha Agosti 11,
2016, pamoja na mambo mengine. Kimeazimia yafuatayo:-
Kuunga
mkono utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuelimisha wananchi
kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa
CCM taifa Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu umuhimu wa kila mwananchi
kudai risiti na muuzaji kutoa risti katika kila manunuzi, kwa lengo la
kuwezesha serikali kupata fedha kupitia kodi, kutoa elimu kwa jamii na
uelewa wa Tanzania yenye viwanda ikiendana na uwanzishaji wa mashamba
darasa ya shirikisho na viwanda vya kati vya kusindika mazao.
Vilevile
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu – CCM, tunafungua milango kwa vijana
mbali mbali wenye lengo la kuunda vikundi vyenye dhamira ya kujikwamua
kiuchumi na kutaka kujiajili, kufika kwenye ofisi zetu za Shirikisho
zilizopo mikoani na Makao Makuu, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam,
ili kupata ushauri wakitaalamu na kusaidiwa kuandika maandiko yatakayo
waongoza kwenye uanzishwaji wa miradi itakayo saidia kutoa fursa za
ajira kwa vijana.
Pia
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu – CCM, linamuomba Mwenyekiti wa CCM,
Rais Dk. John Magufuli, kuwashughulikia kikamilifu wale wote
waliohujumu mali za CCM, kwani vitendo hivyo vinadhoohofisha nguvu ya
chama na wakati mwingine kuwafanya wanachama kuwa wanyonge kwenye Chama
chao.
Shirikisho
la vyuo vya Elimu ya juu – CCM, kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM,
kwa kuhamia Dodoma, tumeazimia kuwa Ofisi ya Makao Makuu ya Shirikisho
nayo itahamia Dodoma rasmi hivi karbuni, baada ya taratibu za
upatikanaji wa Ofisi kukamiliaka.
KUDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano
Shirikisho Makao Makuu
0 comments:
Post a Comment