Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es
Salaam.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai (kulia)
akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu
Damian Lubuva wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto)
akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka
2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar
es Salaam.Picha na Benjamin Sawe-Maelezo
By Christina Njovu
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo
amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job
Ndugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya
kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Akiwa nyumbanikwaspika Jaji Lubuva pia amemkabishiMh. Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwaniya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa
upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali
yakiwemo yale ya biashara SabaSaba na Nanenane katika kutoa elimu kwa
wananchi.
0 comments:
Post a Comment