Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump
Donald
Trump ameeleza mpango wake wa kuifanya Marekani kuwa sehemu salama kwa
kupambana na kile alichokiita kuwa ni ugaidi wa waislamu wenye itikadi
kali. Amesema kama atachaguliwa kuwa rais wa marekani atabadilisha sera
za mamabo ya nje za nchi hiyo zenye lengo la kujenga taifa kwa kuwa na
sera zenye uhalisia.
Akihutubia
mkutano wake katika jimbo la Ohio, mgombea urais kupitia chama cha
Republican alisistiza juu ya umuhimu wa mpango wa muda wa kuzuia viza za
waombaji wanaotoka katika nchi ambazo zina historia ya kueneza ugaidi
,na kupendekeza kuanzishwa kwa
mifumo ya uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa akauti zao za mitandao ya kijamii.
Aidha
bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na nchi yoyote ile
bila kujali tofauti za kiitikadi au mikakati akiwa na nia ya kusaidia
kulitokomeza kundi la Islamic State.
BBC
0 comments:
Post a Comment