Mshambuliaji
mwenye mashuti makali wa timu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, Mussa
Hassan Mgosi, akiwa amembeba mtoto wake, mara baada ya kucheza dakika
tatu, za kuaga kucheza soka kwenye pambano la soka la kirafiki baina ya
timu yake na URA ya Uganda kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam,
Agosti 14, 2016. Mgosi baada ya kuchezea Simba kwa misimu 10 amestaafu
soka na sasa atakua meneja wa timu hiyo. Miongoni mwa watu waliohudhuria
sherehe hiyo ya kustaafu kwake, ni pamoja na Familia yake, mkewe Jasmin
na watoto wake watatu. Katika pambano hilo la kirafiki baina ya Simba
na URA, matokeo yamekuwa sare ya kufungana magoli 1-1. (PICHA NA K-VIS
B;LOG/KHALFAN SAID)
Mgosi
akikokota mpira mbele ya mchezaji wa URL kwenye pambano la soka la
kirafiki kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 14, 2016
Familia
ya Mgosi ikiongozwa na mkewe Jasmina, (katikati) na watoto wake, Amina
(kushoto) na Hassan wakipiga makofi baada ya Mgosi kustaafu soka kwenye
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam
Mchezaji wa Kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo, akiipasua ngome ya URL
Ibrahim Ajib, akikokota mpira
0 comments:
Post a Comment