Miaka 20
tangu simu ya "Smartphone" ilipoingia kwenye soko la mawasiliano, na
kuleta mapinduzi ya kimawasiliano barani Afrika, ambako sasa inatumika
kama chombo cha kupashana habari za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Waafrika
wasiopungua milioni 80 walikuwa na simu ya mkononi mnamo mwaka 1999.
Mwaka 2008 idadi hiyo iliongezeka na kufikia watu 500 milioni - hiyo
ikiwa sawa na asilimia 60 ya wakaazi jumla wa bara la Afrika. Mnamo
mwaka 2015, kwa mujibu wa kamapuni inayotengeneza simu za mkononi chapa
Ericsson, kulikuwa na mikataba takriban bilioni moja ya simu za mkononi
kote barani Afrika.
Wataalam wanakadiria kuna simu bilioni mbili za
mkononi zinazokutikana barani Afrika na katika eneo la Mashariki ya
Kati. Nusu ya simu hizo ni aina ya Smartphones, anasema mkurugenzi wa
kanda ya kusini mwa Afrika wa shirika la kimataifa la Data Corpotration -
IDC, Martin Walker:"Kuendelea kupungua thamani kwa teknolojia ya
Smartphone na kuzidi kuboreka kwa mawasiliano kupitia mtandao pamoja pia
na kuongezeka nguvu za mtandao hadi kufikia 3G na 4G -yote hayo
yamechangia kuifanya Smarthphone izidi kuwavutia watu. Wakati huo huo,
ufundi wa kutengeneza Smarthphone kuambatana na mahitaji ya bara la
Afrika umeongezeka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita."
Smartphone kama chombo cha kuitisha maandamano
Hadi
mwaka 2017, idadi ya Waafrika wanmaotumia simu za mkononi aina ya
Smartphone inatarajiwa kuongezeka mara dufu. Kwa mujibu wa taasisi ya
ushauri wa masuala ya kiuchumi - Deloitte, hadi ifikapo mwakani barani
Afrika kutakuwa na simu zaidi ya milioni 350 za mkononi zenye mtandao wa
intaneti. Hiyo ni fursa kubwa kwa wenye kutengeneza programu za
kibiashara kupitia simu za mkononi na kwa mahitaji ya Waafrika. Hata
hivyo, simu za mkononi hazitumiwi pekee kwaajili ya masuala ya kiuchumi.
Kutokana na kuwepo simu zaidi za mkononi barani Afrika, watu
wanazitumia simu hizo za tekonolojia ya kimamboleo pia kuitisha
maandamano ya kisiasa dhidi ya tawala zao.
Kwa
mujibu wa Professor Marco Manacorda wa Chuo Kikuu cha Queen Mary cha
mjini London, simu za mkononi zinatumika pia kueneza ripoti kuhusu hali
ya kisiasa na kiuchumi kwa haraka zaidi. Anasema kwa kupashana habari
watu wanafanikiwa kujuana pia.
Serikali hazipakati mikono
Prof.
Manacorda anahisi serikali pia zinajifunza jinsi ya kuitumia teknolojia
hiyo mpya ya mawasiliano kama chombo cha upelelezi. Na mara nyingi
wanazifunga njia hizo za mawasiliano.DW
0 comments:
Post a Comment