METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 16, 2016

Sudan Kusini kutathmini azimio la kutumwa askari wa UN Juba

media
 Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Sudan Kusini amesema Jumatatu hii kwamba atatahmini mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutuma askari 4,000 wa kulinda amani katika nchi yake ambayo inakabiliwa na hali ya vurugu kati ya vikosi vya serikali na askari wanaomuunga mkono Reik Machar.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa lilipitisha azimio la kuidhinisha kutumwa kwa kikosi cha ulinzi chenye askari 4,000 katika mji wa Juba kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani nchni humo.

Kikosi hiki, ambacho kinaundwa na askari wa Afrika, kitakua na kazi ya kuhakikisha amani inarejea katika mji mkuu wa Sudan Kusini na kulinda baadhi ya majengo muhimu kama uwanja wa ndege.
Msimamo wa kwanza wa serikali ya Rais Salva Kiir ulikua kufutilia mbali mpango huo kabla ya kurejelea upya msimamo huo mwishoni mwa wiki.

"Baadhi ya watu wanaishtumu serikali ya mpito kukataa na kupambana na Umoja wa Mataifa, jambo ambalo si kweli," amesema Salva Kiir katika sherehe inayoshiria kuanza kwa kikao cha Bunge.

"Serikali ya mpito bado haijakutana ili kueleza uamuzi wake wa mwisho. Majadiliano yatafanyika ili kuamua msimamo wa mwisho," Rais Salva Kiir ameongeza.

Umoja wa Mataifa umetishia Sudan Kusini kuichukulia vikwazo vya silaha kama serikali itakataa kutoa ushirikiano wake.

Shirika la kimataifa la haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa limepata ushahidi wa mauaji ya kikatili ya raia, ikiwa ni pamoja na mauaji ya mwandishi wa habari , aliyeuawa akiwa mikononimwa vikosi vya usalama wakati wa mapigano yalitokea mwezi uliopita. HRW pia imebaini visa vya ubakaji vilivyotekelezwa katika machafuko ya hivi karibuni.

RFI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com