Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amemsimamisha kazi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Captain
Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain Sadick Muze kwa
kosa la kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa
navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa
ajili ya mafunzo ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili
nchini katikati ya mwezi Septemba.
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa
amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili
mpya kwa ajili ya ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo
kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili
ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa
hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
Waziri
Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila
mtumishi wa umma anatekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria kanuni na
taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia
hatua za kinidhamu.
0 comments:
Post a Comment