Muonekano
wa Kivuko cha MV Tanga, kitakachotoa huduma ya usafirishaji katika
Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ambacho ukarabati wake umekamilika tayari
kwa kuanza kazi.
Muonekano
wa Kivuko cha MV Magogoni ambacho ukarabati wake upo katika hatua za
mwisho chenye uwezo wa kubeba tani mia tano, abiria elfu mbili na magari
sitini, kivuko hicho kitaanza kutoa huduma kati ya Magogoni na
Kigamboni katikati ya mwezi huu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga,
amekagua na kuridhika na hatua ya ujenzi na ukarabati wa vivuko vitatu
na tishari moja unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, New MV Magogoni na Tishari litakalotumiwa na Kivuko cha MV Dar es Salaam Eng. Nyamhanga amewapongeza mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Boat Yard Ltd kwa kufanya kazi kwa kasi na ubora unaotakiwa.
“kazi yenu ya ujenzi na ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni, MV Tanga, Kivuko kipya cha Magogoni na Tishari inafanyika kwa viwango vinavyokubalika na hivyo baadae mwezi huu, vivuko vya MV Tanga na MV Magogoni vitaanza kazi, Hongereni”, amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga amesisitiza nia ya Serikali kuhakikisha Ujenzi na Ukarabati wa vivuko unafanyika hapa nchini ili kuzipa nguvu kampuni za kizalendo na kupunguza gharama za utengenezaji na ukarabati nje ya Nchi.
Kukamilika kwa Kivuko cha MV Magogoni chenye uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60 kutapunguza msongamano katika kivuko cha Kigamboni na kuimarisha huduma ya usafiri kati ya Kigamboni na Magogoni.
“Hakikisheni ujenzi wa Tishari na Kivuko kipya cha Magogoni unakwenda kwa kasi, ili kukamilisha mkakati wa Serikali wa kuhuisha usafiri wa majini hapa nchini.” Amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amemhakikishia Katibu Mkuu sekta ya ujenzi kuwa, ushirikiano kati ya TEMESA na kampuni ya Songoro, katika ujenzi na ukarabati wa Vivuko na Tishari ni mzuri na utakamilika kwa wakati.
Kukamilika kwa Kivuko kipya cha Magogoni kunafanya TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa huduma katika maeneo mbalilmbali nchini kote.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga akikagua michoro ya vivuko vitatu na Tishari Moja
ambavyo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho za kukamilika jijini Dar
es Salaam, katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Eng. Manase Ole Kujan.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga akipata ufafanuzi kuhusu hatua za mwisho za ukarabati
wa Kivuko cha Mv Magogoni kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Manase Ole Kujan.
Nahodha
wa Kivuko cha Mv Tanga Bw. Gervas Mahai (katikati), akitoa maelezo
kuhusu mfumo wa uendeshaji wa kivuko hicho ambacho ukarabati wake
umekamilika kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga alipokagua kivuko hicho jijini
Dar esSalaam Kivuko hicho kitapelekwa Pangani wakati wowote kuanzia
sasa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga wa tano kutoka kushoto waliosimama akiwa na wajenzi wa Kivuko cha Mv Tanga na Mv Magogoni kutoka TEMESA na Kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boat Yard Ltd.
0 comments:
Post a Comment