Waziri wa
Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea mbele ya Viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa
nchini(TFDA) hawapo pichani wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya
mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa
kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya
Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa Uzinduzi wa hiyo
leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara za Mamlaka ya Chakula
na Dawa nchini (TFDA )wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka
hiyo leo jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya
ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane
nchini.
Akizungumza
hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya
Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa Afya ,Maendeleo
ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa
Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza
dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.
“Serikali
kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za
binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia
viwanda”.alisema Mhe. Ummy. Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa
kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani
vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza
magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.
Mhe. Ummy
ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini
(TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora
unaopaswa kutumiwa na Watanzania. Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA
inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania
kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .
Mbali na
hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi
zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili
isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo. Kwa upande wa Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea
maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka
na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.
0 comments:
Post a Comment