JESHI la Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 12.
Kamanda
wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, aliwaambia
waandishi wa habari jana kwamba aliyebakwa ni mwanafunzi wa darasa la
tano na ana umri wa miaka 12.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mtuhumiwa huyo ambaye ni mlinzi, Philipo
Stephano , alikamatwa Agosti 2 mwaka huu, saa tisa mchana katika maeneo
ya Soweto, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi mkoani hapa.
“Yule mtoto ambaye jina lake tunalihifadhi, alibakwa na babu yake mzaa mama yake, mkazi wa Soweto.
“Kabla
ya mtuhumiwa kufanya tendo hilo, alimwambia mjukuu wake huyo amwelekeze
na alipokubali, alimpeleka katika eneo analolinda na kumfanyia unyama
huo.
“Baada
ya uchunguzi wa daktari, ilithibitika mwanafunzi huyo alibakwa na
kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri.
“Kwa
hiyo, mtuhumiwa tumemkamata na tunaendelea na upelelezi kabla
hatujampeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Kamanda Mutafungwa.
0 comments:
Post a Comment