Ligi Kuu
ya Uingereza (EPL) imeendelea jana kwa michezo miwili, mchezo wa kwanza
ukiwa ni Crystal Palace iliyokuwa wenyeji wa Liverpool na wapili ulikuwa
West Bromwich waliokuwa nyumbani kuwakabili Manchester United.
Mchezo wa
Liverpool ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2 – 1,
Magoli ya Liverpool yakifungwa na Roberto Firmino dk. 72 na Christian
Benteke dakika ya 90+4 na goli la Crystal likifungwa na Joe Ledley
dakika ya 49.
Mchezo wa
pili wa Manchester United umemalizika kwa wenyeji West Brom kuifunga
Mnchester United goli moja kwa bila, goli lililofungwa na José Rondon
katika dakika ya 67.
0 comments:
Post a Comment