Naibu
Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla amewasimamishwa kazi wauguzi sita
katika hospitali ya Temeke kwa kosa la kuomba rushwa.
Wauguzi
waliosimamishwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe,
Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said, ambao walikuwa zamu
katika wodi ya wajawazito wakati wa tukio hilo.
“Nimewasimamisha
kazi wauguzi wote waliokuwa zamu jana (juzi) asubuhi, nakuagiza Msajili
wa Baraza la Wauguzi uwasimamishe hadi utakapowasafisha kupitia kamati
ya msajili,” alisema Dk Kigwangalla.
Mmoja wa wajawazito, Loshan
Seif alisema alipowasili juzi asubuhi kwa ajili ya kujifungua, muuguzi
mmoja wa zamu alimtaka kulipia Sh5,000 za gloves.
“Siku zote
huwa natumia bima lakini jana (juzi) wakaniambia hawatumii, nitoe
Sh5,000 za gloves, baadaye niliambiwa natakiwa kuwa na uzi wa mshono,
sindano na vingine hivyo kama sina nitoe fedha,” Seif.
Dk Kigwangalla alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo jana saa 9.00 alasiri.
Akizungumza
jana alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo na
kupata malalamiko hayo kutoka kwa wanawake waliojifungua.
“Mama
anaambiwa atoe fedha ya gloves Sh5,000 wakati dukani zinauzwa Sh1,000,
nataka liwe fundisho kwa wote wanaotuongezea vifo vya wajawazito kwa
tamaa ndogondogo,” alisema Kigwangalla.
Katika ziara hiyo, Dk
Kigwangalla alishuhudia ubovu wa vyumba viwili vya upasuaji na kutoa
maelekezo kwamba, virekebishwe ndani ya miezi sita.
“Hali ni
mbaya ndani ya hizi ‘theater’ zote mbili zifanyiwe ukarabati iwapo
itashindikana nitazifunga, lazima ziwe na hadhi yake na nitakuja
kukagua,” alisema.
0 comments:
Post a Comment