METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 10, 2016

DKT JOHN ASHTUKIZA BENKI KUU YA TANZANIA

bt1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016
bt2
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016
bt3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016 

bt4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016
bt5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016
bt6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016
bt7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016 Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.
bt8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akiwa kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao  makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza jana Machi 10, 2016

RAIS John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambako pamoja na mambo mengine, ameiagiza isitishe mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo yaliyokwishaidhinishwa ya zaidi ya Sh bilioni 900, badala yake yarejeshwe Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Aidha, amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wale wote am bao hawana ulazima wa kuwapo.

Vilevile ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.

Rais alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na watendaji wakuu wa Benki wakiwemo, Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja. Kuhusu ulipaji wa malimbikizo ya malipo, wakati Rais Magufuli akisitisha, tayari BoT ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya Sh bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini yafanyike.

Magufuli ameitaka Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kuyapata au la. Kwa upande wa wafanyakazi, Rais Magufuli amemuagiza Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.

“Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani,” alisema Magufuli. BoT imetajwa kuwa ina wafanyakazi 1,391.

Wakati Rais Magufuli akitoa agizo hilo la kutaka orodha ya wafanyakazi ipitiwe upya, Benki hiyo imekuwa ikituhumiwa kuajiri watoto wengi wa vigogo, jambo ambalo liliwahi kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya majina ya vigogo hao yakiwekwa hadharani.

Wakati huo huo, Rais ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com