Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza
na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt
Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya
ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi
10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea
jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea
na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt
Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile
alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam
jana Machi 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga
baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu
wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu
ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10, 2016

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli
akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu
alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius
Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar
es salaam jana Machi 10, 2016
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana
na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango baada ya kufanya ziara
ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam jana Machi 10,
2016 Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa
kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao makuu
ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza jana Machi 10,
2016
Aidha, amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wale wote am bao hawana ulazima wa kuwapo.
Vilevile ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
Rais alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na watendaji wakuu wa Benki wakiwemo, Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja. Kuhusu ulipaji wa malimbikizo ya malipo, wakati Rais Magufuli akisitisha, tayari BoT ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya Sh bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini yafanyike.
Magufuli ameitaka Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kuyapata au la. Kwa upande wa wafanyakazi, Rais Magufuli amemuagiza Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa mara moja wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.
“Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani,” alisema Magufuli. BoT imetajwa kuwa ina wafanyakazi 1,391.
Wakati Rais Magufuli akitoa agizo hilo la kutaka orodha ya wafanyakazi ipitiwe upya, Benki hiyo imekuwa ikituhumiwa kuajiri watoto wengi wa vigogo, jambo ambalo liliwahi kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya majina ya vigogo hao yakiwekwa hadharani.
Wakati huo huo, Rais ameagiza Kitengo cha Madeni ya Nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe BoT mara moja kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni
No comments:
Post a Comment