Jeshi la
Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewatahadharisha wananchi
kutokufanya fujo wakati wa mkesha wa mwaka mpya kwa kuweka mikakati
mikali kwa watakaokaidi amri hiyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku uchomaji wa
matairi ya gari, upigaji baruti, risasi za moto na fataki ambazo zaweza
kusababisha madhara wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
“ Ni
baraka zaidi kusherekea sherehe kama hizi kifamilia na sio vizuri
kuingia mwaka mpya ukiwa mahabusu, huo ni mkosi” Alisema Kamishna Kova.
Kamishna
Suleiman Kova aliongeza kuwa watashirikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni
pamoja na Jeshi la Zimamoto, kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya
ulinzi shirikishi pamoja na kutumia ndege za Polisi kufanya doria ili
kuhakikisha kuwa wanailinda amani na kudhibiti aina yoyote ya uhalifu
utakaojitokeza.
Aidha
Kamishna Kova amesisitiza kuwa vituo vyote vya polisi vitakuwa wazi
masaa 24 ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa haraka pindi wanapopata
matatizo au wanapoona dalili zozote za uvunjifu wa amani pia
amehakikisha kuwa fukwe zote za bahari na maeneo yote yenye mikusanyiko
yatalindwa.
0 comments:
Post a Comment