Icon wa muziki Afrika Naseeb ‘Diamond’ Abdul, amemmwagia sifa mzazi mwenzie Zarina ‘Zari’ Hassan kuwa anasifa zote za mke mwema.
Plutnumz amesema mara nyingi Zari
amekuwa ni mwanamke anayependa kupika tofauti na wale aliokuwa nao hapo
kabla. “Yani kiukweli Zari ni mwanamke fulani ambaye ni wa kipekee sana,
hapendi kabisa ninachokula kipikwe na mtu mwingine, kitu kinachonihusu
kifanywe na mtu mwingine.
Hana gubu mnaweza mkagombana lakini
ukiingia ndani tayari ugomvi umekwisha kabisa, akikaa jikoni baada ya
muda mfupi tu anatoa kitu fasta” Alisema Diamond.
Katika ‘line’ nyingine mkali huyo alidai, Mungu akipenda muda si mrefu watafunga pingu za maisha.
0 comments:
Post a Comment