METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, November 26, 2015

Balozi Mahiga mwenyekiti UDOM Rasmi




Balozi Augustine Mahiga (Kushoto)  Balozi Juma

Balozi Agustine mahiga kushoto balozi mwampachu

Balozi maige ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa chuo kikuu cha dodoma (UDOM) Kuziba nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na balozi Mwapachu.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana makamu mkuu wa chuo hicho profesa Idris Kikula alisema balozi mwapachu alikuwa amemaliza muda wake tangu septemba 30 mwaka huu.

Pia amesema mkuu wa chuo hicho Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa amemuongezea muda wa miezi 6 makamu wa chuo hicho ,mipango,Fedha na utawala profesa shaban mlacha aliyekuwa amalize muda wake disemba 30 mwak huu.

 Alisema uamuzi huo unataka kumpa nafasi ili amalize miladi aliyokuwa ameianzisha ukiwamo wa umeme wa jua.

Profesa kikula alisema profesa mlacha na naibu mkuu wa chuo taaluma,utafiti na ushauri profesa ludovick kinabo walimaliza muda wao mwaka jana lakini waliongewa mwaka mmoja.

Alisema utalatibu wa kuwapata watu watakao ziba nafasi hizo mbili ulioanza miezi miwili iliyopita umeshafanyika.

kwa upande wa mahafari profesa alisema wahitimu 4,136 wakada na nafasi mbalimbali  watatunukiwa vyeti.

Alisema idadi hiyo imeongezeka ukilinganisha na ya mwaka jana ambayo wahitimu walikuwa 3,949.

Amesema tangu kuanzishwa chuo hicho wahimu waliohitimu wamefikia idadi ya watu 26,663

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com